Ama baada ya hayo, itambulike kuwa shirki ndio dhuluma aina kubwa. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

“Hakika shirki ni dhulma kubwa mno!”[1]

Yule mwenye kufa juu ya shirki hapati msamaha wa Allaah. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[2]

Pepo imeharamishwa kwa mshirikina maharamisho ya milele. Amesema (Ta´ala):

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ

“Hakika yule mwenye kumshirikisha Allaah, bila shaka Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni.”[3]

Mshirikina ni najisi ambaye si halali kwake kuingia Makkah. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا

“Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu.”[4]

Damu na mali ya mshirikina ni halali. Amesema (Ta´ala):

فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ

“Itapomalizika miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, wafanyeni mateka na wahusuruni na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru.”[5]

Mshirikina amepotea upotevu wa wazi na amezua dhambi kubwa mno. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ

“Yeyote anayemshirikisha Allaah basi ni kana kwamba ameporomoka kutoka mbinguni wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno.”[6]

Si halali kumuozesha mshirikina. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ

“Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.”[7]

Mshirikina matendo hayakubaliwi kutoka kwake wala ´ibaadah anazofanya hazisihi. Amesema (Ta´ala):

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Hakika umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako na hakika utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[8]

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[9]

Tunaomba ulinzi kwa Allaah kutokamana na mashaka, shirki, kufuru, unafiki, tabia mbaya na mageuko mabaya katika mali, ahli na watoto.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wak wote.

[1] 31:13

[2] 04:48

[3] 05:72

[4] 09:28

[5] 09:05

[6] 22:31

[7] 02:221

[8] 39:65

[9] 06:88

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 43-47
  • Imechapishwa: 03/04/2019