13- Kufariki kwa maradhi ya kifua kikuu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kufa katika njia ya Allaah ni shahada, mwanamke mwenye damu ya uzazi ni shahada, kuungua kwa moto ni shahada, kuzama ndani ya maji ni shahada, maradhi ya kifua kikuu ni shahada na kufa kwa maradhi ya tumbo ni shahada.”

Imesemwa katika “al-Majma´ az-Zawaaid” (02/317) na (05/301):

“Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”, kutoka kwa Salmaan. Ndani yake yumo Mandalu bin ´Aliy. Juu yake kuna maneno mengi na amefanywa kuwa ni mwaminifu.”

Lakini hata hivyo inatolewa ushahidi na Hadiyth ya Raashid bin Hubaysh ambayo nimetangulia kuiashiria katika “alama ya kumi”. Ahmad amezidisha katika upokezi wake:

“… na maradhi ya kifua kikuu.”

Wapokezi wake wamefanywa kuwa ni waaminifu na al-Mundhiriy amewafanya kuwa ni wazuri. Ina Hadiyth zengine zinazoisimamishia ushahidi katika “al-Majma´” kutoka katika Hadiyth ya ´Ubaadah bin as-Swaamitw na ushahidi wa tatu kutoka katika Hadiyth ya ´Aaishah iliopo kwa Abu Nu´aym katika “Akhbaar Aswbahaaniy” (01/217-218).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 04/02/2020