29. Ndio maana haiyumkiniki Qur-aan ikawa imeumbwa


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

kwa sababu Qur-aan inatokamana na Allaah na chenye kutokamana na Allaah hakikuumbwa.

MAELEZO

Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa majina na sifa Zake ndiye Muumbaji. Kila kisichokuwa Yeye kimeumbwa. Haifai kusema kwamba majina na sifa za Allaah vimeumbwa. Vinatokamana na Allaah. Chenye kutokamana na Allaah hakikuumbwa. Kwa msemo mwingine ni kuwa Allaah anasifika nazo. Allaah kwa majina na sifa Zake ndiye Muumbaji. Vyengine vyote mbali na Yeye vimeumbwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 70
  • Imechapishwa: 22/01/2018