28. Msimamo wa watawala wa waislamu hapo kale kwa wazushi


al-Ja´d bin Dirham alipouawa akaja baada yake al-Jahm bin Swafwaan. Yeye pia akaanzisha imani yake chafu. Akauawa na Salm bin Ahwaz[1]. Namna hii ndivo walivyokuwa watawala wa waislamu. Walikuwa wakiwaua mazanadiki kwa ajili ya kuilinda ´Aqiydah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuibadilisha dini yake muueni.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Si halali damu ya mtu muislamu isipokuwa kwa moja ya mambo matatu; ambaye kishawaingia kuingia katika ndoa akazini, nafsi inauliwa kwa nafsi nyingine au anayeiacha dini yake mwenye kufarikisha al-Jamaa´ah.”[3]

Walikuwa wakiwaua mazanadiki na wakiwastarehesha waislamu kutokamana na shari yao kwa ajili ya kuilinda ´Aqiydah ambayo ndio jambo la kwanza la kilazima katika yale mambo matano ya kilazima ambayo ni wajibu kwa kuyahifadhi.

Hili ndio chimbuko la imani hii mbaya. Kisha Mu´tazilah wakairithi. Ja´fariyyah katika Shiy´ah pia wanaamini imani yao. Kwa sababu walijifunza kutoka kwa Mu´tazilah na wakajifunza kutoka kwao. Shiy´ah az-Zaydiyyah na Ibaadhiyyah wanaamini imani hii na wanaitakidi kuwa Qur-aan imeumbwa na kwamba sio maneno ya Allaah. Wote haya wameyarithi kutoka kwa Jahmiyyah. Yote haya yameandikwa katika ´Aqiydah zao wanazosoma hivi sasa.

[1] Tazama ”Bayaan Talbiys-il-Jahmiyyah” (01/277) na ”Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah”, uk. 591.

[2] al-Bukhaariy (6922, 3017) kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

[3] al-Bukhaariy (6878) na Muslim (1676) kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 49
  • Imechapishwa: 15/03/2021