Swali 28: Baadhi ya wafanyakazi kwenye sekta ya afya katika kazi yao wanalazimika kuchanganyikana na mwanamke ambaye ni kando na wao na khaswa mwishoni mwa usiku kwenye kitengo cha waliolazwa kwenye ICU wakiwa ndani ya ofisi za madakktari wataalam. Wakati wa kuwanasihi juu ya udharurah wa kutatua tatizo hilo basi wanaelekeza lawama zote kwa wahusika. Tunaomba utupe maelekezo na nasaha juu ya hali kama hizi.

Jibu: Ni wajibu wasimamie hayo wanaume ambao ni waaminifu. Kukihitajika wanawake basi ni lazima wawe kundi la wanawake ili kusitokee faragha. Kundi la wanawake wasiwe chini ya wawili. Wanawake hawa wawe upande wao na wanaume wawe upande wao, madaktari wa kike wawe na wagonjwa wao wa kike na vivyo hivyo upande wa wanaume. Haifai kwa mwanaume kukaa faragha na mwanamke ambaye ni ajibaki kwake. Si mchana wala usiku. Haifai kwa daktari wa kike wala mwengine kukaa faragha na daktari wa kike au muuguzi wa kike. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume hakai faragha na mwanamke isipokuwa watatu wao anakuwa ni shaytwaan.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 15/10/2019