Swali 27: Ni ipi hukumu ya mwenye kubadilisha/kusafisha damu kwa ambaye ni mgonjwa wa figo ilihali amefunga? Ni lazima kulipa siku hiyo?

Jibu: Ni lazima kulipa kwa sababu ya ile damu safi inayotoka. Kukizidi juu ya hapo nyenzo zengine basi hivo vitakuwa ni vifunguzi vyengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 30
  • Imechapishwa: 11/05/2019