27. Mafunzo yanayopelekea katika manufaa, utukufu na kufaulu


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Nimeshakupa mfano wa yale yanayowanufaisha ikiwa watayahifadhi, watatukuka wakiyajua na watafurahi wakiyaitakidi na kuyatendea kazi.

MAELEZO

Nimeshakutajia katika utangulizi wa kitabu hiki yale ambayo wanafunzi wakiyahifadhi na wakayafahamu basi yatawanufaisha, watapata utukufu wa elimu na matendo na furaha muda wa kuwa watayaamini na kuyatendea kazi, tofauti na vile vitabu vya ´Aqiydah ambavyo havibainishi ´Aqiydah ya Salaf, kama vile ´Aqiydah za wanafalsafa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 26
  • Imechapishwa: 13/07/2021