Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kila kisichokuwa Allaah ni walimwengu [kimeumbwa] na mimi ni mmoja katika walimwengu hao.

MAELEZO

Walimwengu ni kila kisichokuwa Allaah. Wamepata jina hili kwa sababu wao ni alama juu ya Mola, Mmiliki Wao na Mwendeshaji wao. Katika kila kitu kuna alama inayojulisha kuwa Yeye ni Mmoja.

Mimi pia ni mmoja katika walimwengu hao. Mambo yakishakuwa hivo kwamba Yeye ndiye Mola Wangu, basi ni lazima kwangu kumwabudu Yeye peke Yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 47
  • Imechapishwa: 20/05/2020