10- Mwanamke kufa katika damu yake ya uzazi kwa sababu ya kuzaa kwake. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Ubaadah bin as-Swaamitw aliyesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtembelea ´Abdullaah bin Rawaah. Hakuondoka kwenye kitanda chake mpaka akasema: “Unawajua mashahidi ni wepi wa Ummah wangu?” Wakasema: “Muislamu kufa kwa kuuawa ni kufa shahidi.” Akasema: “Basi mashahidi wa Ummah wangu watakuwa wachache; kufa kwa tauni ni kufa shahidi, mwanamke anayekufa kwa sababu ya mtoto wake ambaye bado yuko tumboni mwake ni kufa shahidi [mtoto wake atamvuta kwa kitovu chake kumwingiza Peponi].”

Ameipokea Ahmad (04/201-05/323), ad-Daarimiy (02/208), at-Twayaalisiy (582) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Ina ushahidi katika “al-Musnad” (04/315, 317, 328) na “at-Taariykh Ibn ´Asaakir” (08/436/02) njia zengine.

Katika maudhui haya ipo Hadiyth kutoka kwa Swafwaan bin Umayyah kwa ad-Daarimiy (01/289), an-Nasaa´iy (01/289) na Ahmad (06/465) – 466).

Kutoka kwa ´Uqbah bin ´Aamir kwa an-Nasaa´iy (02/62-63) na kwa al-Bukhaariy katika “at-Taariykh” (03/01/58) qadhiya inayohusu kuzama ndani ya maji.

Kutoka kwa Raashid bin Hubaysh kwa Ahmad (03/289) na wapokezi wake ni waaminifu. al-Mundhiriy amesema katika “at-Targhiyb” (02/201):

“Cheni ya wapokezi wake ni nzuri na ndani yake kuna ziada. Nayo ni ile Hadiyth ya ´Ubaadah kwa at-Twayaalisiy na ´Ahmad. Pia kutoka kwa ´Abdullaah bin Busr kwa at-Twabaraaniy. Wapokezi wake ni waaminifu kwa al-Haythamiy (05/301).

Kutoka kwa Jaabir bin ´Atiyk na kutakuja tamko lake katika alama ya inayofuata:

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 04/02/2020