26. Sifa na majina ya Allaah yaliyothibiti katika Qur-aan VI

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.” (03:55)

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ

”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.” (04:158)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.” (35:10)

يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَأَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Ee Haamaan! Nijengee mnara mkubwa ili nifikie njia. Njia za mbinguni ili nimchungulie Mungu wa Muwsaa, kwani hakika mimi namdhania ni muongo.” (40:36-37)

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

”Je, mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu] kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu] kwamba Hatokutumieni kimbunga [cha mawe], basi mtajua vipi [makali] maonyo Yangu.” (67:16-18)

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

”Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anajua yanayoingia ardhini, na yatokayo humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo – Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo. Na Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuyaona.” (57:04)

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

”Hauwi mnong’ono wa [watu] watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala [hauwi mnong’ono wa] chini kuliko ya hivyo, na wala wa wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa; kisha Atawajulisha kwa yale [yote] waliyoyatenda Siku ya Qiyaamah – hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi daima.” (58:07)

لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا

“Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.” (09:40)

إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

”Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.” (20:46)

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

”Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa na wale ambao wao ni wema.”

(16:128)

وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ

”Subirini. Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri.” (08:46)

كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ

“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.” (02:249)

MAELEZO

Aayah hizi zilizotajwa na mwandishi (Rahimahu Allaah):

1- Kuna zinazozungumzia kuhusu Ujuu.

2- Zingine zinahusiana upamoja.

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amejithibitishia Mwenyewe Ujuu na kwamba yuko juu ya ´Arshi, yuko juu ya mbingu (Jalla wa ´Alaa) na kwamba anaombwa kutokea kwa juu. Ahl-us-Sunnah wameafikiana juu ya hilo. Ahl-us-Sunnah wameafikiana ya kwamba Allaah (Subhaanah) yuko juu na kwamba yuko juu ya ´Arshi na kwamba amelingana kulingana ambako kunalingana na Utukufu na Ukubwa Wake. Amesema (Subhaanah):

Dalili ya kwamba Allaah amelingana juu ya ´Arshi Yake

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa Rahmah amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

Kuna Aayah saba ambazo zote (Subhaanah) amethibitisha Ujuu na kwamba amelingana juu ya ´Arshi (Jalla wa ´Alaa). Ni kulingana ambako kunalingana na Utukufu Wake. Hafanani na viumbe Vyake katika kitu chochote katika sifa Zake. Ni dalili yenye kuonyesha Ujuu. Kwa ajili hii ndio maana (Jalla wa ´Alaa) amesema:

Dalili ya kwamba Allaah yuko juu ya viumbe Vyake kwa dhati Yake

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.”(03:55)

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ

”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.”(04:158)

Bi maana ´Iysaa (´alayhis-Salaam).

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.” (35:10)

Neno “kupanda” na “kunyanyuliwa” ni dalili yenye kufahamisha Ujuu. Matendo hupandishwa na neno zuri hunyanyuliwa Kwake.

Vilevile Malaika hupanda Kwake. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

“Malaika na Roho [Jibrily] wanapanda Kwake katika siku kiasi chake ni miaka khamsini elfu.” (70:04)

Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipandishwa Kwake mpaka akapita tabaka ya saba na akasikia maneno ya Mola (Jalla wa ´Alaa). Yote haya ni haki kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni wajibu kumthibitishia Allaah. Amesema (Subhaanah):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

”Je, mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu] kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu] kwamba Hatokutumieni kimbunga [cha mawe], basi mtajua vipi [makali] maonyo Yangu.”(67:16-18)

Maana ya “mbinguni” (fis-Samaa´), bi maana juu. Naye ni Allaah (Jalla wa ´Alaa). Imesemekana vilevile ya kwamba “as-Samaa´”, maana yake ni zile mbingu. Kadhalika maana ya “fiy” yaani juu. Kwa hivyo maana yake inafika inakuwa juu ya mbingu. Ikisemwa kuwa “mbingu” maana yake ni juu maana yake inakuwa wazi. Hivyo inakuwa ya kwamba (Jalla wa ´Alaa) yuko juu. Vilevile ikisemwa “mbingu” maana yake ni zile mbingu zilizojengwa maana yake inakuwa ´yuko juu ya mbingu`. Kwa sababu “fiy” wakati mwingine inakuja ikiwa na maana ya “juu”. Amesema (Ta´ala) kuhusu Fir´awn:

وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ

“Nitakusulubuni (fiy) katika mashina ya mitende.” (20:71)

Bi maana juu ya mashina ya mitende.

Vilevile amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ

“Basi tembeeni (fiy) katika ardhi.” (09:02)

Bi maana juu ya ardhi.

Kwa hivyo kusema kuwa Allaah yuko mbinguni maana yake ni kwamba yuko juu yake na Yeye (Jalla wa ´Alaa) yuko juu ya kila kitu. Haya ndio maoni ya Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa yuko juu na kwamba yuko juu ya ´Arshi. Hili ni tofauti na watu wa Bid´ah miongoni mwa Khawaarij, Mu´tazilah, Jahmiyyah na wengineo. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amejithibitishia Mwenyewe kuwa juu na kwamba yuko juu ya ´Arshi.

Ahl-ul-Bid´ah ndio wenye kusema kuwa Allaah yuko kila mahali. Huu ni ujinga, batili na kufuru. Wanayoamini Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wenye kuwafuata kwa wema ni kwamba Yeye (Subhaanah) ni Mwenye kusifika kuwa juu ya ´Arshi na kwamba amelingana juu yake, kwa msemo mwingine amengatika juu yake kungatika ambako kunalingana na Utukufu Wake. Hafanani na viumbe Vyake katika kitu katika sifa Zake.

Wakati Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah), ambaye alikuwa ndiye mwanachuoni mkubwa wa al-Madiynah katika wakati wake, alipoulizwa juu ya hili akajibu kwa kusema:

“Kulingana kunajulikana. Namna haijulikani. Kuamini hilo ni wajibu. Kuuliza kuhusu hilo ni Bid´ah.”

Vivyo hivyo imepokelewa kutoka kwa mwalimu wake Rabiy´ah bin Abiy ´Abdir-Rahmaan, Umm Salamah, al-Awzaa´iy, ath-Thawriy, Ishaaq bin Raahuuyah, Imaam Ahmad bin Hanbal na maimamu wengine wa Salaf.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com