26. Msingi wa nane: Msimamo wetu kwa watawala madhalimu

8- Kulazimiana kwetu na yale yaliyofahamishwa na Qur-aan, Sunnah na wakaafikiana kwayo Salaf katika namna ya kutangamana na viongozi na watawala wetu

Tunasikiza na kutii katika yasiyokuwa maasi[1]. Hatuonelei kufaa kufanya uasi kwa mtawala muislamu. Haijalishi kitu ni maasi mengi kiasi gani atakuwa nayo. Hatuingilii chochote katika mambo ya dunia yao. Tunawanasihi kwa mujibu wa njia ya ki-Shari´ah kwa ukweli na kumtakasia nia Allaah. Nasaha inatakiwa kutolewa kwa siri na khaswakhaswa katika zama za fitina.

Tunawaombea kwa Allaah kutengamaa katika hali yetu ya usiri na ya dhahiri. Kwa sababu wao wakitengamaa ndio kutengamaa kwa waja na miji.

Tunachukia kuingia kwenye majumba yao isipokuwa kwa lengo la nasaha au kupeleka mashtaka ya kudhulumiwa.

Tunaonelea kupigana jihaad bega kwa bega pamoja nao.

Tunawakemea wale wenye kuwatukana na kuwaanika mbele za watu. Kwa sababu kitendo hicho kinawachochea raia dhidi yao, jambo ambalo linaweza kupelekea katika moja ya mambo mawili:

1- Kufanya uasi dhidi yao.

2- Kuasi amri ya ki-Shari´ah.

Hapa nitanukuu maneno ya maimamu wa Da´wah (Rahimahumu Allaah) katika “ad-Durar as-Saniyyah” (07/177-178). Shaykh na ´Allaamah ´Abdul-Latwiyf bin ´Abdir-Rahmaan bin Hasan bin Muhammad Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahumu Allaah) amesema:

“Hapa kuna masuala mengine na janga kubwa ambalo shaytwaan amewadanganya kwalo watu wengi. Matokeo yake wakawa wanajaribu mambo yanayotenganisha umoja wa waislamu, yanawajibisha tofauti katika dini, yanayosemwa vibaya na Kitabu kinachoweka wazi, likapelekea kumwagika damu ardhini, kuachwa jihaad na kumnusuru Mola wa walimwengu, likapelekea kuzuiwa kwa zakaah, kuamsha moto wa fitina na upotevu. Shaytwaan akajipenyeza kuingiza vitimbi hivi na kuziwekea hoja na vitangulizi na akawafanya kuelewa makosa kwamba kuwatii baadhi ya walioshinda kimabavu – bi maana miongoni mwa watawala – katika yale aliyoamrisha Allaah na Mtume Wake katika yale mambo ambayo ni lazima kumfanyia kiongozi, kuzuia kwa ajili ya Uislamu na kulinda milki zake katika hali hii ni jambo ambalo si la lazima na wala halikusuniwa.”

Ufupisho wa vitimbi ni kwamba kuwatii baadhi ya watawala walioshinda kwa mabavu ni jambo ambalo si la lazima katika hali ya fitina na wala halikusuniwa.

Kisha Shaykh akasema akiwa ni mwenye kuraddi vitimbi hivi:

“Watu hawa waliopewa mtihani hawajui kuwa waislamu wengi tokea wakati wa Yaziyd bin Mu´aawiyah –  mbali na ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz na wale aliotaka Allaah miongoni mwa Banuu Umayyah – kulitokea kwao yaliyotokea katika mambo ya kimabavu, matokeo mbalimbali makubwa, uasi na maharibifu katika uongozi wa waislamu. Pamoja na hivo historia ya maimamu wa ulimwengu na viongozi wakubwa pamoja na watawala ni mashuhuri na yenye kutambulika. Walikuwa hawaondoshi mkono kutoka katika utiifu katika yale aliyoamrisha Allaah na Mtume Wake katika Shari´ah za Uislamu na yale mambo ya dini ambayo ni wajibu.”

Kisha akayapigia hayo mifano kwa kusema:

“Hebu nikupigie mfano wa hayo kwa al-Hajjaaj bin Yuusuf ath-Thaqafiy. Jambo lake lilienea kwa watu kutokana na dhuluma, kuchupa mipaka katika kumwaga damu, kukiuka maharamisho ya Allaah, kuwaua watu watukufu wa Ummah kama mfano wa Sa´iyd bin Jubayr, akamzingira Ibn-uz-Zubayr, kuzuiwa watu kuingia msikiti mtakatifu wa Makkah, akahalalisha heshima, akamuua Ibn-uz-Zubayr, licha ya kuwa Ibn-uz-Zubayr alimtii na akapewa kiapo cha utiifu na watu wote wa Makkah, Madiynah, Yemen na watu wengi wa ´Iraaq. Kipindi hicho al-Hajjaaj alikuwa ni naibu wa Marwaan na mtoto wake ´Abdul-Malik. Hakuna yeyote katika makhaliyfah wala Ahl-ul-Hall wal-´Aqd aliyekula kiapo kwa Marwaan. Pamoja na hivo hakuna yeyote katika wanachuoni ambaye alijizuia kumtii, kumnyenyekea katika yale ambayo inafaa kumtii katika mambo yanayohusiana na nguzo na mambo ya wajibu ya Uislamu.

Ibn ´Umar na wengineo waliokutana na Maswahabah wengine wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliokutana na al-Hajjaaj hawakuwa wakipingana naye, wakijizuia kumtii katika yale mambo yenye manufaa kwa Uislamu na yenye kuikamilisha imani. Vivyo hivyo wale Taabi´uun waliokuwa katika wakati wake. Kwa mfano Ibn-ul-Musayyib, al-Hasan al-Baswriy, Ibn Siyriyn, Ibraahiym at-Taymiy na wengineo mfano wao katika viongozi wa Ummah. Hali iliendelea namna hiyo kati ya wanachuoni wa Ummah kutoka kwa viongozi na maimamu wa Ummah. Walikuwa wakiamrisha kumtii Allaah na Mtume Wake, kupambana jihaad katika njia yake bega kwa bega pamoja na kila kiongozi. Ni mamoja kiongozi huyo ni mwema au muovu. Hayo yanatambulika katika vitabu vya misingi ya dini na vya ´Aqiydah.

Vivyo hivyo Banuul-´Abbaas walitawala miji ya waislamu kwa nguvu baada ya kushinda kwa upanga. Hakuna yeyote katika wanachuoni na watu wenye dini waliowasaidia. Waliua viumbe wengi katika Banuu Umayyah, viongozi wake na manaibu wake. Pia walimuua Ibn Hubayrah ambaye alikuwa kiongozi wa ´Iraaq na wakamuua khaliyfah Marwaan. Mpaka ikanakiliwa kwamba katili kwa siku moja aliua karibu watu thamanini katika Banuu Umayyah ambapo akaweka magodoro juu ya mizoga yao na akaitisha vyakula na vinywaji.

Pamoja na haya yote historia na msimamo wa maimamu mfano wa al-Awzaa´iy, Maalik, az-Zuhriy, al-Layth bin Sa´d, ´Atwaa´ bin Abiy Rabaah kwa watawala hawa ni wenye kujulikana kwa yule ambaye anajishughulisha na elimu na kusoma.

Tabaka la pili la wanachuoni kama vile Ahmad bin Hanbal, Muhammad bin Ismaa´iyl, Muhamamd bin Idriys, Ahmad bin Naswr, Ishaaq bin Raahuuyah na ndugu zao watawala katika zama wao walitumbukia katika Bid´ah kubwakubwa kama mfano wa kupinga sifa za Allaah, kuita watu katika jambo hilo, wakawapa watu mtihani kwa jambo hilo, baadhi wakauliwa akiwemo Ahmad bin Naswr, pamoja na haya yote haitambuliki kuwa kuna yeyote miongoni mwao ambaye aliondosha mkono wake kutoka katika utiifu wala kuona kuwa inafaa kuwafanyia uasi.”

Akaendelea mpaka pale Shaykh (Rahimahu Allaah) aliposema:

“Ukipatwa kifuani mwako na chochote katika kigugumizi basi kithirisha kumnyenyekea Allaah, kufanya Tawassul kwa zile du´aa zilizopokelewa na kusoma kwa wingi yale yaliyotajwa na historia ya Ibn Ghanaam kutoka katika maneno ya Shaykh-ul-Islaam – yaani Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab – kwani hakika ameyazungumzia masuala haya kwa undani ndani ya vitabu na dondoo zake.”[2]

[1] Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas (Rahimahu Allaah) ana vitabu vitatu kuhusu maudhui haya:

1- Mu´aamalat-ul-Hukkaam fiy Dhwa´-il-Kitaab was-Sunnah.

2- ´Aqiydatu Ahl-is-Sunnah fiymaa yajib lil-Imaam.

3- al-Amr biluzuum Jamaa´at-il-Muslimiyn wa imaamihim wat-Tahdhiyr min mufaaraqatihim.

[2] ”ad-Durar as-Saniyyah fiy al-Ajwibat-in-Najdiyyah” (08/377-380).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 62-67
  • Imechapishwa: 15/10/2020