26. Imani ya al-Ja´d bin Dirham kwamba Qur-aan sio maneno ya Allaah kaitoa kwa mayahudi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Naamini kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah. Yameteremshwa na hayakuumbwa.

MAELEZO

Ilipokuwa miongoni mwa misingi na nguzo za imani ni kuamini Vitabu ambavyo Allaah ameviteremsha kwa Mitume Yake kwa ajili ya kuwaongoza waja, kuhukumu kati yao katika yale waliyotofautiana kwayo na kusimamisha hoja juu yao. Amesema (Ta´ala):

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ

“Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah akawatuma Mitume hali ya kuwa ni wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu kati ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo.”[1]

Amesema (Ta´ala) kumwambia Mtume wetu Muhammad (´alayhis-Salaam):

وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ

“Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua.”[2]

إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا

”Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa haki ili uhukumu kati ya watu kwa aliyokuonyesha Allaah; wala usiwe mtetezi kwa makhaini.”[3]

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

“Tumekuteremshia Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao na huenda wakapata kutafakari.”[4]

Wakati ilipokuwa Qur-aan aliyoteremshiwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni maneno ya Allaah kama ilivyo kwa Vitabu vyengine vya kiungu na kwamba kuamini hayo ni nguzo moja wapo miongoni mwa zile nguzo sita za imani, kitu ambacho waislamu wote wameafikiana juu yake. Lakini baada ya kumalizika karne bora kujitokeza imani fulani kupitia kwa al-Ja´d bin Dirham ambaye alijifunza ´Aqiydah yake kutoka kwa mayahudi ambaye alikuwa anasema kuwa Qur-aan imeumbwa kwa sababu Allaah hazungumzi – Allaah ametakasika kutokamana na wanayoyasema utakasifu mkubwa. Alikuwa anaona kuwa maneno kuegemezwa Kwake ni uegemezaji wa kimafumbo. Kwa sababu Allaah aliyaumba maneno ndani ya mwengine. Allaah aliyaumba kwenye Ubao uliohifadhiwa, ndani ya Jibriyl au ndani ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ametakasika Allaah! Ni vipi ataegemeza maneno kwenda kwa ambaye hakuyazungumza? Akili haikubali kitu kama hiki. Ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa kwenye akili. Malengo yao kwa kusema hivo ni kubadilisha jambo la kutumia Qur-aan kama dalili na waseme kuwa hakuna kati ya watu maneno ya Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 02:213

[2] 04:113

[3] 04:105

[4] 16:44

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 47
  • Imechapishwa: 15/03/2021