Shaykh Bakr amesema:

“Katika moja ya kichwa cha khabari kwenye yaliyomo kuna “Sayyid Qutwub anasema kuwa Qur-aan imeumbwa na kwamba maneno ya Allaah ni ibara ya Utashi”. Niliporejea huko sikuona neno hata moja ambapo Sayyid Qutwub (Rahimahu Allaah) anaashiria kwa kusema kimatamshi:

“Qur-aan imeumbwa.”

Ni vipi mtu kwa urahisi anaweza kumtuhumu mtu kwa kufuru hizi? Kikubwa nilichoona ni pindi alipofunga katika usulubu wake kwa mfano pindi aliposema:

“Hawawezi kutunga kwavyo – yaani herufi za kukata – mfano wa kitabu kama hichi. Kwa sababu ni katika uundaji wa Allaah na sio wa binaadamu.”

Hatuna shaka kuwa ibara hii ni ya kimakosa, lakini kupitia sentesi hii kuhukumu kuwa Sayyid Qutwub anazungumza kwa madhehebu ya kikafiri ya kwamba Qur-aan imeumbwa sikubaliani nalo.”[1]

Inaonekana kuwa Shaykh Bakr anaanguka vipande vipande kwa sababu ya kuwa na ghera na hamasa kwa Sayyid Qutwub. Sikuona kwake athari yoyote ya ghera ya Sunniy Salafiy juu ya ´Aqiyah ya Kiislamu ambayo amesafisha Sayyid kwa kukanusha na kupotosha Sifa.

Hatukuona athari yoyote juu ya Nabii wa Allaah Muusa ambaye Allaah alimsemeza.

Hatukuona ghera yoyote juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kadhalika.

Ni kwa sababu gani? Kuna sira zepi nyuma ya hili?

Kwa ghera na hamasa yake kubwa mtu huyu anafanya yote ili kumtetea Sayyid na kumtakasa ili awafurahishe Qutbiyyuun, makhurafi na watu mfano wao na watu wa Bid´ah wengine ambao wanamtukuza Sayyid Qutwub pamoja na kuwashambulia wale wenye kujaribu kuingilia utakasifu wa mtu huyu.

Katika mlango huu Shaykh Bakr anavaa mavazi ya Dhwaahiriyyah wameshikilia herufi na matamko na kupuuza malengo na maana. Hatimae Sayyid Qutwub anakuwa ni mwenye kutakasika kutokamana na ´Aqiydah hii kama Imaam Ahmad.

Naweza kuwa nimekosea nikisema kuwa ni katika Dhwaahiriyyah katika suala hili. Huenda yuko na vitabu vya Sayyid Qutwub ambapo anawaraddi wale wenye kusema kuwa Qur-aan imeumbwa. Huenda vilevile akawa yuko na makala ambapo anawaraddi wale wenye kusema kuwa Qur-aan imeumbwa na wengineo. Kuna uwezekano vilevile akawa ameshafanya hivo katika vitabu vyake ambavyo vimeenea ulimwenguni kote na mimi sijaona hilo. Yote haya yanawezekana na kwamba yote hayo, au baadhi yake, pamoja na unyenyekevu mkubwa, yamemfanya Shaykh Bakr kumtakasa. Natumai nitaokolewa kutokamana na makosa makubwa yote haya niliyofanya pindi nilipomdhulumu na kufanya ujasiri kwa Sayyid Qutwub.

Hata hivyo asipopata kitu, basi namuomba msomaji, na khaswa msomaji Salafiy, anipe udhuru.

Msomaji anatakiwa atambue kuwa miaka ishirini iliyopita mimi tayari nilikuwa nimeshapata jinsi Sayyid Qutwub anavyotamka wazi kuwa Qur-aan ni uundaji wa Allaah na kwamba imeundwa. Pamoja na hivyo sikusema kwamba amesema kuwa Qur-aan imeumbwa isipokuwa baada ya kukusanya dalili zenye nguvu na za wazi kutoka katika maneno ya Sayyid na historia yake ndio yaliyonifanya mimi kumsifu kwa sifa hii kwa ajili ya kuwanasihi waislamu na kufichua fikira za watu wa Bid´ah.

[1] Uk. 03-04