25. Ni kweli kwamba vitabu vya Ruduud ni vitabu vya fitina na visienezwe?


Swali 25: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kuwa kitabu “Qutwbiyyah” ni cha fitina na haijuzu kukitawanya kwa vijana?

Jibu: Kitabu “Qutwbiyyah” ndani yake mna uzinduzi juu ya makosa yaliyotokea. Kuzindua juu ya makosa yaliyotokea ni jamb la wajibu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewaamrisha waja Wake mjuzi mwenye kulijua jambo basi amzindue asiyejua. Kwa mfano Allaah amesema kuhusu Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam):

وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ

“Akaja mtu kutoka pande ya mbali ya mji ule akiwa anakimbia akasema: “Ee Muusa!  Hakika wakuu wanashauriana dhidi yako ili wakuue basi toka [ukimbie] hakika mimi kwako ni miongoni mwa wanaonasihi.”” (28:20)

Mtu huyu amekuja anakimbia kwa ajili ya kumnasihi Muusa kutoka katika mji huo wa watu ambao walikuwa wakishauriana juu ya kumuua. Mtu huyu alipofanya hivi alifanya kitendo cha kheri au kibaya? Ni kitendo cha kheri. Allaah (´Azza wa Jall) alikuwa anataka Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) awe Mtume mtukufu katika wale waliokuwa na subira sana na Allaah awahidi watu kupitia yeye baada ya hapo. Mtu huyu aliyekuja kumnasihi alifanya kitendo cha kheri na kizuri. Je, inaweza kusemwa kuwa amezua fitina? Kadhalika inahusiana na mtu ambaye sasa atawazindua watu na wanafunzi juu ya watu wanaowatakia shari. Wanachotaka ni wao wawafanyia uasi watawala wa waislamu. Allaah (Subaanahu wa Ta´al) ameharamisha juu yao kufanya hivo. Waonyaji hawa ni wenye kuwanasihi ndugu zao.

Kutokana na haya tunapata kujua kuwa kitabu “Qutwbiyyah” sio cha fitina. Mtu au watu hawa wanaosema hivi maneno yao ni batili na wamekosea. Wao ndio watu wa fitina. Wao wanachotaka ni kunyamazia batili ili wafikie jambo lao na wapotevu waweze kufanya uasi na hapo ndio chanzo cha damu kumwagika, watu kufa, heshima kuvunjika, njia kuvunjwa na yatokee yakutokea kwa sababu ya kuwafanyia uasi watawala na kufanya jambo ambalo Allaah (Ta´ala) ameharamisha.

Ni jambo lisilo na shaka mtu ambaye anawazindua watu juu ya shari kabla haijatokea ni mwenye kuwapendea kheri na sio mlinganizi wa fitina. Mwenye kusema maneno haya amepindua uhakika wa mambo. Fitina ni kule kunyamazia mfano wa matendo kama haya ili watu hawa ambao wana nia mbaya waweze kufikia malengo yao. Je, hapo nasaha tena nasaha zitafaa? Mfano ikiwa utajua kuna mtu anataka kulipua na kuunguza mahala na ukajua kuwa mtu huyu ni dhalimu au wanaotaka kufanya hivo ni watu wa batili, basi ni wajibu kwako kuwanasihi walengwa ili watahadhari. Kwa hivyo kuzindua juu ya shari kabla haijatokea haizingatiwi kuwa ni katika fitina. Huku ni kutaka kupindua uhakika wa mambo. Tunamuomba Allaah  awaondoshee utata walio nao kwenye nyoyo zao na mambo ambayo kwayo wanapindua uhakika wa mambo na kuyafanya yaonekana kuwa ni batili.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017