Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

20- Alikuwa na sifa ya uungu wakati hapakuwa yeyote wa kuabudu, alikuwa ni Muumbaji wakati hapakuwa kiumbe yeyote.

MAELEZO

Alikuwa ni Mola kabla ya kuwepo viumbe. Mola maana yake ni mmiliki, mwendeshaji, mtengenezaji na bwana; sifa hizi hazitengani na dhati Yake. Ni Mwenye kusifiwa uungu pasi na mwanzo wala mwisho. Alikuwa hivo kabla ya kupatikana viumbe na ataendelea kuwa hivo baada ya viumbe kutokomea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 44
  • Imechapishwa: 18/09/2019