25. al-Qummiy upotoshaji wa nne wa al-Baqarah


al-Qummiy amesema:

“Amesema:

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ

“Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile na wala haitakubaliwa kutoka kwake uombezi na wala hakitachukuliwa kutoka kwake kikomboleo na wala hawatanusuriwa.” (02:48)

“Amesema (´alayhis-Salaam)[1]: “Ninaapa kwa Allaah ya kwamba lau kila Malaika aliye karibu na Mtume aliyetumwa amuombea Naaswib hatoitikiwa [uombezi wake].”[2]

Hata kama Aayah hii inawagusa wengine pia hata hivyo inawazungumzisha mayahudi. Kwa nini amewapuuzisha mayahudi? Ameipotosha Aayah na kuilenga kwa wale ambao Raafidhwah wanaita kuwa ni “Naaswibah”, bi maana Maswahabah na kila mwenye kuwafuata inapokuja katika imani ya kweli, Tawhiyd na kuwaheshimu watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanawafanya kuonekana kama maadui wakubwa wa Allaah kuliko mayahudi na manaswara. Wanawapachika Aayah za ukafiri na Moto juu yao.

Ninaapa kwa Allaah kuwa si ´Aliy wala mwingine kutoka katika kizazi chake kitukufu hakuna aliyesema haya. Huu ni uzushi tu wa wanafiki Raafidhwah.

[1] Pengine ni Abu ´Abdillaah.

[2] Tafsiyr al-Qummiy (01/48).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 57
  • Imechapishwa: 19/03/2017