24. Viongozi wa mashirika wawape ruhusa wafanyakazi wanaotoa nyudhuru za uongo?


Swali 24: Baadhi ya wafanyakazi hukwepa kazi zao kwa sababu ya anakuwa na maslahi yake mengine ya kibinafsi mbali ile kazi yake. Kwa hivyo anamuomba ruhusa meneja wake na anatoa nyudhuru ambazo mara nyingi zinakuwa sio zenye kukinaisha. Je, meneji huyu anapata dhambi kwa kumkubalia ikiwa anajua kwamba nyudhuru hizo si sahihi?

Jibu: Haijuzu kwa meneja wa idara au mkurugenzi au ambaye anasimama nafasi yake akakubaliana juu ya kitu ambacho anaamini kuwa si sahihi. Bali ni lazima kwake kupeleleza. Ikiwa kuna dharurah ya kumpa ruhusa kwa sababu ya haja kubwa na wakati huohuo kumpa ruhusa hakuidhuru kazi hakuna neno. Kuhusu nyudhuru ambazo anajua kuwa ni za uongo au ana dhana yenye nguvu ya kwamba ni za uongo, basi ni lazima kwa meneja wake asimpe udhuru na wala asimkubalie. Kwa sababu hivo ni kufanya khiyana katika kazi na kuvunja uaminifu kwa wale waliomwamini na waislamu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nyote ni wachungi na nyote mtaulizwa juu ya kile mlichokichunga.”

Hii ni amana. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

“Hakika Allaah anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe.”[1]

Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala) juu ya sifa za waumini:

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ

“Ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga.”[2]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

”Enyi walioamini! Msimkhaini Allaah na Mtume na wala msikhaini amana zenu na hali nyinyi mnajua.”[3]

[1] 04:58

[2] 23:08

[3] 08:27

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 47
  • Imechapishwa: 09/10/2019