7- Kufunga mwezi wa Allaah Muharram. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swawm bora baada ya Ramadhaan ni mwezi wa Allaah Muharram. Na swalah bora baada ya faradhi ni swalah ya usiku.”[1]

8- Kufunga siku tisa za Dhul-Hijjah. Siku hizi zinaanza tarehe moja ya Dhul-Hijjah na inamalizika siku ya tisa ambayo ni siku ya ´Arafah. Hayo ni kutokana na kuenea kwa Hadiyth zilizopokelewa juu ya fadhilah za matendo ndani yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna masiku ambayo matendo mema yanapendwa zaidi na Allaah kama siku hizi kumi.”[2]

Funga pia ni katika matendo mema.

[1] al-Bukhaariy (1976).

[2] Muslim (1163).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 163
  • Imechapishwa: 01/05/2020