Yakishatambulika haya ni kwamba ni jambo limethibiti kutokana na yale yanayojulikana katika Uislamu kwa njia ya ulazima ya kwamba hakuna dini isipokuwa kwa kuwepo mkusanyiko, kama ambavo hakuna mkusanyiko isipokuwa kwa kuwepo kiongozi, kama ambavo hakuna kiongozi isipokuwa mpaka kuwepo jambo la kusikiliza na kutii. ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hakuna Uislamu isipokuwa kwa mkusanyiko, hakuna mkusanyiko isipokuwa kwa uongozi na wala hakuna uongozi isipokuwa kwa utiifu.”[1]

Shaykh na ´Allaamah Bakr Abu Zayd amesema katika kitabu chake nimetoka kukiashiria punde kidogo:

“Hiki ndicho kinachopata kufahamika kwa mujibu wa Shari´ah juu ya mkusanyiko wa waislamu. Ni wenye kujenga  udugu juu ya mfumo wa kinabii (Qur-aan na Sunnah). Kiongozi mwenye nguvu na mwenye uwezo wa kuzuia ndiye anayewaongoza. Haya ndio mafungamano yenye kuenea kati ya waislamu kwa ajili ya umoja, kushikamana na mkusanyiko wao. Hutokea tofauti na mparanganyiko wa mambo kwa kadri na vile watavyozembea. Ikiwa mmoja katika waislamu atajitoa nao au pote, basi huku ni kuleta mpasuko kati ya waislamu, kufarikisha umoja wao na jambo hilo – katika maumbile ya hali yake – ni kujiondoa nje ya Uislamu mzima kwa mujibu wa mfumo wa kinabii.”[2]

[1] ad-Daarimiy katika ”as-Sunnah” yake (01/315) (257).

[2] ”Hukm-ul-Intimaa´ ilaal-Firaq”, uk. 36.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 15/10/2020