24. Baada ya kutwahirika na damu ya uzazi ameanza kuona tena damu

Swali 24: Mwanamke baada ya kutwahirika kwa damu ya uzazi miezi miwili ameanza kupata baadhi ya matone madogo ya damu. Je, aache kufunga na asiswali?

Jibu: Matatizo ya wanawake kuhusu hedhi na damu ya uzazi ni bahari isiyokuwa na ufukwe. Miongoni mwa sababu za matatizo hayo ni wanawake kutumia vidonge vya kuzuia mimba na kuzuia hedhi. Watu hapo kabla hawakuwa wanatambua matatizo haya mengi. Ni kweli kwamba matatizo yalikuweko tokea hapo alipotumilizwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), bali tangu hapo walipopatikana wanawake. Lakini yamekuwa mengi kwa njia hii inayomfanya mtu anasimama hali ya kuwa amechanganyikiwa katika kutatua matatizo yake, jambo ambalo linasikitisha.

Lakini kanuni ilioenea ni kwamba mwanamke akisafika na akaona usafi wenye uhakika katika hedhi na katika damu ya uzazi. Ninachokusudia kusafika na hedhi ni kutoka kwa ule mtiririko mweupe. Mtiririko mweupe ni maji meupe wanayajua wanawake. Umanjano, maji ya uchafuchafu, tone au unyevu yanayotokea baada ya kutwahirika, hali zote hizi hazizingatiwi kuwa ni hedhi. Hivyo hali hizo hazimzuii kuswali, kufunga wala mwanamme kumjamii mkewe. Kwa sababu sio hedhi. ´Umm ´Atwiyyah amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na maji ya uchafuchafu kuwa ni kitu.”

Ameipokea al-Bukhaariy. Abu Daawuud anayo nyongeza:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na maji ya uchafuchafu kuwa ni kitu baada ya kutwaharika.”

Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

Kujengea juu ya haya tunasema kwamba kila kitachotokea katika hali hizo zilizotangulia baada ya utwahirifu ambao ni wenye uhakika basi hayamdhuru mwanamke na wala hayamzuii kutokamana na swalah, kufunga na mume wake kukutana naye. Lakini mwanamke anatakiwa asifanye haraka mpaka aone kutwahirika. Baadhi ya wanawake pindi damu inawakauka basi papohapo wanakimbia kuoga kabla ya kuona kuwa amesafika. Kwa ajili hii wanawake wa Maswahabah walikuwa wakimtumia mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) pamba ilio na damu na hivyo anawaambia wasiharakishe mpaka waone mtiririko au maji meupe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 10/07/2021