24. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Maswahabah

Lililo la wajibu kwa Maswahabah ni kuwapenda, kuwasifia, kuwafuata, kuwaigiliza na kutoingilia yale yaliyopitika kati yao kipindi cha fitina. Ee muumini! Kamwe usiingie ndani ya mambo haya na usiyazungumzie. Usiwatie makosani baadhi yao na ukawafanya wengine kupatia. Kwa sababu walikuwa ni wenye kujitahidi (Radhiya Allaahu ´anhum) na wakilenga haki. Ni lazima kwako kuuzuia ulimi wako na usiwazungumzie. Ni lazima kuhifadhi juu yao wasia wa Allaah (Jalla wa ´Alaa) na wasia wa Mtume Wake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msiwatukane Maswahabah wangu. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake lau mmoja wenu atatoa dhahabu kiasi cha mlima wa Uhud basi hatofikia viganja viwili vilivyojazwa na mikono vya mmoja wao wala nusu yake.”[1]

“Allaah Allaah juu ya Maswahabah wangu. Msiwafanye lengo baada yangu.”[2]

Kuwapenda Maswahabah ni katika kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye kuwapenda Maswahabah amempenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mwenye kuwachukia Maswahabah amemchukia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huu ndio wajibu juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anhum).

Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bukhaariy (3273) na Muslim (2541) kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh). Ameipokea vilevile Muslim (2540) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

[2] at-Tirmidhiy (3762), Ahmad (05/45, nambari. 2059) kupitia kwa ´Abdullaah bin Mughaffal (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 44
  • Imechapishwa: 11/03/2021