Swali 23: Kuna mtu amepatwa na maradhi ya ukimwi na madaktari wamethibitisha kuwa umri wake uliobaki wa kuishi ni mfupi sana. Ni ipi hukumu ya tawbah yake katika mnasaba kama huu?

Jibu: Ni juu yake kukimbilia kufanya tawbah hata kama ni katika wakati wa kifo. Kwa sababu mlango wa tawbah umefunguliwa vovyote hali ilivyo midhali mtu bado yuko na akili yake. Ni lazima kwake kuharakisha kufanya tawbah na kujiepusha na maasi. Haijalishi kitu hata kama wamesema umri wake ni mfupi. Miaka ya watu iko mikononi mwa Allaah. Jengine wanaweza kukosea kwa kudhania kwao na matokeo yake akaishi maisha marefu. Kwa hali yoyote ni lazima kukimbilia kufanya tawbah na awe mkweli katika jambo hilo ili Allaah apate kumsamehe. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Tubuni kwa Allaah nyote, enyi waumini, ili mpate kufaulu.”[1]

وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ

”Hakika Mimi ni Mwingi mno wa kusamehe kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema kisha akaendelea kuongoka.”[2]

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anaikubali tawbah ya mja muda wa kuwa hajakuwa katike ile hali ya kukata roho.”

Maana ya hali hii ni ile ambayo mtu anahisi alama ya kifo.

[1] 24:31

[2] 20:82

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 46
  • Imechapishwa: 03/10/2019