4- Kufunga jumatatu na alkhamisi kila wiki. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitilia umuhimu funga ya jumatatu na alkhamisi.”[1]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Matendo huonyeshwa jumatatu na alkhamisi. Hivyo napenda yaonyeshwe matendo yangu nami nimefunga.”[2]

5- Kufunga siku tatu kila mwezi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Abdullaah bin ´Amr:

“Funga katika mwezi siku tatu. Kwani hakika jema moja linalipwa mara kumi mfano wake na hivyo ni kama kufunga mwaka mzima.”

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Aliniusia kipenzi changu mambo matatu; kufunga siku tatu kila mwezi, Rak´ah mbili za Dhuhaa´ na kuswali Witr kabla ya kulala.”

Masiku hayo yamependekezwa yawe yale meupe; tarehe 13, 14 na 15. Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi mwenye kufunga katika mwezi basi afunge siku tatu nyeupe.”

6- Kufunga siku moja na kuacha ya kufuata. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Swawm bora ni ya Daawuud (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akifunga siku moja na akila ya kufuata.”

Hii ndio funga iliyopendekezwa ambayo ni bora zaidi.

[1] Ahmad (05/201) na at-Tirmidhiy (745) ambaye amesema:

“Nzuri na Swahiyh”.

Ameisahihisha al-Albaaniy katika “Ta´liyq ´alaa Ibn Khuzaymah” (2116).

[2] at-Tirmidhiy (751), an-Nasaa´iy (01/322), Abu Daawud (2432).  Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (596).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 162-163
  • Imechapishwa: 01/05/2020