120- ´Aliy, Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ´Ikrimah, Mujaahid na Muhammad bin Ka´b al-Qaradhwiy (Rahimahu Allaah) wamesema pindi walipokuwa wakifasiri maneno Yake (Ta´ala):

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.” (16:97)

“Bi maana kukinaika.”

121- Allaah (Ta´ala) alisema kumwambia Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ

“Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.” (07:144)

122- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Amefaulu yule mwenye kusilimu, akaruzukiwa kuwa na utoshekaji na Allaah akamkinaisha kwa vile alivyompa.”[1]

123- Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Muusa (´alayhis-Salaam) amesema: “Ee Mola! Waja wako wema kabisa ni wenye alama zipi?” Allaah (Ta´ala) akamfunulia: “Ni wenye kukinaika kwa kidogo na anajihifadhia vingi kwa ajili ya Aakhirah.”

124- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaadamu hana haki yoyote isipokuwa zifuatazo: nyumbani anakoeshi, nguo anazofunika viungo vyake vya siri na mkate na maji.”[2]

[1] Muslim (1054).

[2] at-Tirmidhiy (3444) ambaye ameisahihisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 79-84
  • Imechapishwa: 18/03/2017