23. Du´aa wakati wa deni


116- ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba kuna mtumwa mmoja alikuja na kujaribu kujinunua huru kwake na kusema: “Mimi siwezi nashindwa kujinunua huru. Nisaidie.” Akasema: “Nisikufunze maneno aliyonifunza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Lau utakuwa na deni mfano wa jibali Allaah Atakulipia nalo. Sema:

اللهُمَّ اكْفِنِي بِحَلاَلِكَ عنْ حَرامِكَ وأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سوَاكَ

“Ee Allaah! Nitosheleze mimi kwa halali yako kutokana na haramu yako. Nitajirishe kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine usio Wewe.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 21/03/2017