Kuhusu Tawassul zilizokatazwa ni kule kufanya Tawassul kwa dhati za viumbe, haki na jaha zao. Kama mfano mtu aseme: “Nakuomba kupitia fulani”, “Nakuomba kwa haki ya fulani”, “Nakuomba kwa jaha ya fulani”. Ni mamoja kiumbe huyo yuhai au ameshakufa. Hizi ni Bid´ah zilizoharamishwa na ni njia zinazopelekea katika shirki. Yule mwenye kufanya hivo akijikurubisha kwa kiumbe anayemfanyia Tawassul hiyo kwa kumtekelezea aina yoyote ya ´ibaadah, basi hiyo ni shirki kubwa. Kama mfano wa kumchinja kwa ajili ya walii, kuliwekea nadhiri kaburi, kumwita, kumuomba uokozi na mengineyo. Tunamuomba Allaah awape uelewa waislamu wa dini yao, awanusuru dhidi ya maadui zao na awaongoze wale waliopotea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 40
  • Imechapishwa: 01/04/2019