22. Sifa na majina ya Allaah yaliyothibiti katika Qur-aan IV

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ

“Je, wanangojea [nini] isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika na itolewe hukumu?” (02:210)

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ

”Je, wanangojea jingine [lolote] isipokuwa wawafikie Malaika [kuwatoa roho] au awafikie Mola wako au ziwajie baadhi za alama za Mola wako?” (06:158)

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

”Sivyo hivyo! [Kumbukeni pale] ardhi itakapovunjwavunjwa. Na Atakapokuja Mola wako, na Malaika safu kwa safu.” (89:21-22)

وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا

”Na [kumbusha] Siku itakayopasuka mbingu kwa [kutoa] mawingu; na Malaika watateremshwa mteremsho wa wingi.” (25:25)

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”Kila aliyekuwa humo [mbinguni na ardhini] ni mwenye kutoweka. Na utabakia Uso wa Mola wako Mwenye Utukufu na Ukarimu.” (55:27)

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.” (28:88)

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75)

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ
”Na Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” [Siyo, bali] mikono yao ndio iliyofumbwa; na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali Mikono Yake imefumbuliwa Hutoa Atakavyo.” (05:64)

وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا

”Na subiri kwa hukumu ya Mola wako, kwani hakika wewe uko kwenye Macho yetu.”(52:48)

وَحَمَلْنَاهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

”Na Tukambeba kwenye ile [jahazi] iliyo [tengenezwa] kwa mbao na misumari. Inatembea kwa Macho Yetu.” (54:13-14)

وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِّنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي

”Na Nikakutilia mahaba kutoka Kwangu na ili ulelewe Machoni Mwangu.” (20:39)

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ

”Allaah Amekwishasikia kauli ya yule [mwanamke] anayejadiliana nawe kuhusu mumewe na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (58:01)

 

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ

”Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale [Mayahudi] ambao wamesema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri”.” (03:181)

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ

”Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! [Tunasikia!] Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.” (43:80)

إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

”Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.” (20:46)

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ

”Je, hajui kwamba Allaah Anaona?” (96:14)

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ

”Na mtegemee Mwenye nguvu kabisa, Mwenye kurehemu – Ambaye Anakuona wakati unaposimama.” (26:217-218)

وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ

”Na sema [uwaambie]: Fanyeni [mtakavyo]. Allaah Ataona ‘amali zenu na Mtume Wake, na Waumini.” (09:105)

وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ

”Naye ni Mkali wa kusibu misiba na maangamizi.” (13:13)

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

”Na wakapanga njama, lakini Allaah Akapanga [kuwalipiza] njama. Na Allaah ni Mbora wa kurudisha njama za wenye kupanga njama.” (03:54)

وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

”Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama [zao kwa kuwaadhibu], nao huku hawatambui.” (27:50)

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًاوَأَكِيدُ كَيْدًا


”Hakika wao wanapanga njama
Nami napanga mipango [ya kuvunja na kupindua njama zao].” (86:15-16)

Dalili ya Kusamehe, Kurehemu na Uwezo wa Allaah

إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا

”Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu; basi hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Muweza.” (04:149)

وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Na wasamehe na waachilie mbali. Je, [nyinyi] hampendi Allaah Akusameheni? Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (24:22)

وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ

”Na hali utukufu ni wa Allaah na wa Mtume Wake na wa Waumini.” (63:08)

فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

“Naapa kwa Utukufu Wako, bila shaka nitawapotosha wote.”(38:82)

 

تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

Limebarikika Jina la Mola wako – Mwenye Utukufu na Ukarimu.”(55:78)

فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

”Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua [mwengine] mwenye Jina Lake? (19:65)

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Na wala hana yeyote anayefanana [kulingana] Naye.” (112:04)

MAELEZO

Aayah zote hizi tukufu ndani yake mna jumla ya sifa kwa Mola (´Azza wa Jall). Ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah (Subhaanah) kwa njia inayolingana Naye pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kuzilinganisha. Miongoni mwazo ni pamoja na Kauli Yake (Jalla wa ´Alaa):

Dalili ya Kuja na Kuwasili kwa Allaah

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ

“Je, wanangojea [nini] isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika na itolewe hukumu?” (02:210)

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

“Na Atakapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”(89:22)

Ni kuhusu kuja kwa Allaah siku ya Qiyaamah. Kuja siku ya Qiyaamah ni haki kwa njia inayolingana na Allaah. Allaah hashabihiani na viumbe Vyake kwa chochote katika sifa Zake. Amesema (Ta´ala):

أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ

”… au ziwajie baadhi za alama za Mola wako”(06:158)

Ni kuchomoza kwa jua kutoka magharibi.

Dalili ya Uso wa Allaah

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

Na utabakia Uso wa Mola wako – Mwenye Utukufu na Ukarimu.”(55:27)

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.” (28:88)

Hapa kuna uthibitisho wa Uso wa haki. Ni Uso mtukufu.

Dalili ya Mikono ya Allaah

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali Mikono Yake imefumbuliwa.” (05:64)

Allaah anasifika kuwa na mikono kama ambavyo vilevile Ana uso mtukufu (Jalla wa ´Alaa).

Dalili ya Allaah kuwa na Macho

Kadhalika anasifika kuwa na macho. Amesema (Ta´ala):

وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي

“Na ili ulelewe Machoni Mwangu.”(20:39)

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

Inatembea kwa Macho Yetu.” (54:14)

Anasifika kuwa na macho na usikizi kwa njia inayolingana na Yeye (Subhaanah). Sifa zote hizi ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia inayolingana Naye.

Vivyo hivyo inahusiana na kufanya njama. Ni jambo limefungamanishwa na mkabala:

Dalili ya Adhabu na njama za Allaah

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ

”Na wakapanga njama, lakini Allaah Akapanga [kuwalipiza] njama.” (03:54)

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًاوَأَكِيدُ كَيْدًا

”Hakika wao wanapanga njama Nami napanga mipango [ya kuvunja na kupindua njama zao].” (86:15-16)

Ni njama zinazolingana na Allaah. Hafanani na viumbe Wake katika kupanga Kwake njama Zake.

Vivyo hivyo inahusiana na usikizi. Amesema (Ta´ala):

Dalili ya Kusikia na Kuona kwa Allaah

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا

”Allaah Amekwishasikia kauli ya yule [mwanamke] anayejadiliana nawe kuhusu mumewe na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu.” (58:01)

إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

“Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi.” (02:181)

إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ

“Hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”(58:01)

Kuna Aayah nyenginezo nyingi zenye kuthibitisha usikizi, ujuzi na uoni.

Vilevile kuna Aayah nyingi zenye kuthibitisha kupenda. Zote hizo ni haki na ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia yenye kulingana Naye.

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua [mwengine] mwenye Jina kama Lake?” (19:65)

 

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

  “Na wala hana yeyote anayefanana [kulingana] Naye.” (112:04)

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

 
”Basi msipigie mifano Allaah! Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.”(16:74)  

Zote hizi ni [sifa za] haki na ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa njia inayolingana na Allaah pasi na upotoshaji, ukanushaji na kuzipindisha maana. Ana usikizi na sio kama usikizi wetu, ana uoni na sio kama uoni wetu, macho sio kama macho yetu, mkono sio kama mkono wetu, nguvu na sio kama nguvu zetu. Hali kadhalika inahusiana na sifa zingine zote. Anasema (Subhaanah):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

Sifa zake ni haki na ni zenye kulingana na Yeye. Sifa Zake hazifananishwi na viumbe Vyake (Jalla wa ´Alaa). Ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia yenye kulingana Naye bila ya kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna wala kuzifananisha. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa mlango ni mmoja. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com