22. al-Qummiy na al-´Ayyaashiy upotoshaji wa al-Baqarah

al-Qummiy amesema wakati alipofasiri Kauli ya Allaah (Ta´ala):

الم ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ

Alif Laam Miym. Hiki ni Kitabu – kisicho na shaka ndani yake – ni uongofu kwa wachaMungu.” (02:01-02)

“Imepokelewa ya kwamba Abu ´Abdillaah (´alayhis-Salaam) amesema: “Kitabu ni ´Aliy ambaye hakuna shaka ndani yake na uongofu kwa wachaMungu ni ubainifu kwa wafuasi wetu.”[1]

al-´Ayyaashiy amesema:

“Sa´daan bin Muslim amepokea kutoka kwa baadhi ya marafiki zake, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema: “Kitabu hichi ni Kitabu cha ´Aliy ambacho hakuna shaka ndani yake na wachaMungu ni wafuasi wetu:

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ

“Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.” (02:03)

Bi maana wanatendea kazi yale tuliyowafunza.”[2]

Mhakiki amesema kwenye taaliki:

“al-Bihaar (21/21), al-Burhaan (01/53) na as-Swaafiy (01/58-59).”

Namna hii ndivyo Raafidhwah wanavofasiri Kitabu cha Allaah, Kitabu ni ´Aliy ambaye hakuna shaka ndani yake na wachaMungu ni Shiy´ah. Wakati huo huo Maswahabah na waumini wengine wote ni wenye kufukuzwa, wapotevu, walioghadhibikiwa, wanafiki na watu wa Motoni kwa mujibu wa Raafidhwah.

[1] Tafsiyr al-Qummiy (01/30)

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/25-26)

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 55
  • Imechapishwa: 19/03/2017