Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Itakapokuwa mtu hayuko hivo apuuze viwili hivyo [Qur-aan na Sunnah] kwa ulazima huo na hilo halina shaka yoyote. Na mwenye kutafuta uongofu katika hivyo [Qur-aan na Sunnah], basi ima ni zindiki au ni mwendawazimu kutokana na ugumu wa kuvifahamu. Kutakasika kutokamana na mapungufu ni kwa Allaah na himdi zote njema ni stahiki Yake. Ni mara ngapi Allaah amebainisha Kishari´ah na ki-Qadar, kimaumbile na kiamri, akijibu utata huu uliolaaniwa kwa njia mbalimbali zilizofikia kiwango cha ulazima wa ujumla:

وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Lakini watu wengi hawajui.” (07:187)

لَقَدْ حَقَّ الْقَوْلُ عَلَىٰ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلَالًا فَهِيَ إِلَى الْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ وَجَعَلْنَا مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَاهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ وَسَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ وَخَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ بِالْغَيْبِ ۖ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ

“Hakika imethibiti kauli [ya adhabu] juu ya wengi wao, kwa hiyo hawaamini. Hakika Sisi tumeweka kwenye shingo zao minyororo, ikawafika videvuni [hawawezi kufanya kitu]; kwa hivyo vichwa vyao vimeinuliwa. Na tumeweka mbele yao kizuizi na nyuma yao kizuizi, hivyo tukawafunika, basi wao hawaoni. Na ni mamoja kwao, ukiwaonya au usiwaonye hawaamini. Hakika wewe unamuonya yule anayefuata ukumbusho na akamkhofu Mwingi wa rehema kwa ghaibu, basi mbashirie msamaha na ujira mtukufu.” (35:07-11)

MAELEZO

Aayah hizi zinawahusu wale wenye kupuuza kuyazingatia maneno ya Allaah na ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwisho wake ni yule aliyeneemeshwa na Allaah:

مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ وَخَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ

“… yule anayefuata ukumbusho na akamkhofu Mwingi wa rehema.” (35:11)

Huu ndio mfano wa watu aina mbili hawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 43
  • Imechapishwa: 19/05/2021