21. Dalili ya kumi na tisa kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

19-  Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy ametukhabarisha: Hamad bin Ahmad al-Haddaad ametuhadithia: Ahmad bin ´Abdillaah ametuhadithia: Muhammad bin al-Mudhaffar ametuhadithia: Ahmad bin ´Umayr ametuhadithia: ´Aliy bin Ma´bad bin Nuuh ametuhadithia: Swaalih bin Bayaan ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Abbaas aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja hukimbilia haja miongoni mwa haja za duniani ambapo Allaah juu ya mbingu saba anamkumbuka na kusema: “Malaika wangu. Mja wangu huyu anakimbilia haja miongoni mwa haja za duniani. Nikimfungulia basi nitamfungulia mlango miongoni mwa milango ya Motoni. Lakini muwekeni mbali nayo.” Hivyo mja anauma meno vidole vyake na kusema: “Ni nani aliyenitangulia?  Ni nani aliyenitia adabu?” Mambo yalivyo si vyengine isipokuwa ni rehema ambayo Allaah amemrehemu.”

Hadiyth hii ni geni kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Mujaahid. Abu Nu´aym amesema:

“Hatukuiandika isipokuwa kutoka kwa ´Aliy bin Ma´bad, kutoka kwa Swaalih.”[1]

[1] Hilyat-ul-Awliyaa’ (3/305). adh-Dhahabiy amesema:

“Swaalih ameharibika. Shu´bah hakusimulia haya.” (al-´Uluww, uk. 44)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 03/06/2018