20. Sio wajibu kuzifasiri sifa za Allaah

81- Majina na sifa za Allaah (Ta´ala) hazifahamiki kwa kutumia akili, kwa sababu akili inaweza tu kutambua sifa ilizoona au kuona mfano wake. Allaah (Ta´ala) hazungukwi na maono na wala Hana anayefanana Naye. Kwa hivyo majina na sifa Zake haziwezi kutambulika isipokuwa kupitia Qur-aan na Sunnah. Katika Qur-aan na Sunnah majina na sifa zimetajwa pasi na kutaja namna wala tafsiri zake. Kwa hivyo mtu anatakiwa kushikamana na kufupika na yale yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Kwa sababu hakuna ujuzi zaidi ya huo, jengine ni kwa sababu imeharamishwa kumsemea Allaah kitu pasi na elimu. Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [aina zote] na ukandamizaji bila ya haki. Na [ameharamisha] kumshirikisha Allaah kwa ambayo hakukiteremshia mamlaka na kuzungumza juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[1]

82- Ikiwa tamko linaweza kuwa na maana nyingi na kukatumiwa maana moja bila ya kulenga dalili, kuna khatari ya kwamba si lenye kuafikiana na makusudio ya Allaah (Ta´ala). Matokeo yake mtu anakuwa amemsifu Allaah kwa kitu ambacho hakujisifu nacho Mwenyewe. Matokeo mengine ni kwamba anamkanushia Allaah kitu ambacho amejisifu nacho Mwenyewe. Kwa hivyo yanapatikana makosa mawili wakati mmoja. Aidha amezungumza juu ya Allaah kwa asiyoyajua, amepekua kitu ambacho hakulazimishwa na ameenda kinyume na njia iliyopitwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake na Salaf na badala yake ameshika njia ya Jahm na mazanadiki na wapotevu wenzake.

83- Kufasiri sio jambo la wajibu kwa maafikiano. Kwa sababu ingelikuwa ni wajibu basi maana yake ni kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake waliacha kitu cha wajibu na wakakusanyika juu ya batili.

84- Yule mwenye kusoma Qur-aan na asijue maana yake hapati dhambi. Hakuna tofauti juu ya hili. Ikiwa haya ni kwa yule mwenye kusoma Qur-aan basi ni aula zaidi kutomuwajibikia yule asiyesoma.

85- Lau tafsiri ingelikuwa wajibu kwa kila mmoja basi ingelikuwa ni makalifisho yasiyowezekana. Hiyo pia ingepelekea mtu asiyekuwa msomi kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Kidhibiti kiko vipi endapo ingelikuwa ni wajibu kwa baadhi tu?

[1] 07:33

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 19/12/2018