20. Kujisalimisha na Qadhwaa pasina kushindwa na kutelekeza

Allaah (Ta´ala) Amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗوَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

“Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kwa ndugu zao; waliposafiri katika ardhi au walipokuwa vitani: “Lau wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wala wasingeliuawa,” ili Allaah Afanye hayo (yaliyoeleweka vibaya) majuto katika nyoyo zao. Na Allaah Anahuisha na Anafisha. Na Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona yote daima).” (Aal ´Imraan 03 : 156)

112- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendwa zaidi na Allaah (Ta´ala) kuliko muumini dhaifu – na kwa wote wawili mna kheri. Pupia juu ya yale yenye kukupa manufaa. Omba msaada kwa Allaah (´Azza wa Jalla) na usishindwe. Ukifikwa na kitu usiseme: “Lau ningelifanya hivi ingelikuwa kadhaa na kadhaa”. Badala yake sema: “Allaah Amekadiria na Alipendalo hufanya.” Hakika “lau” hufungua matendo ya Shaytwaan.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 21/03/2017