2. Uwajibu wa kuingia katika Uislamu

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kutoka kwake, naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (03:85)

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

“Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.” (03:19)

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Hii ndio njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate vichochoro [vinginevyo]; vikakufarikisheni na njia Yake!” (06:153)

Mujaahid amesema:

“Vichochoro ni Bid´ah na utata.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuzusha katika amri yetu hii yasiyokuwemo yatarudishwa.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Yule mwenye kufanya tendo lisiloafikiana na amri yetu litarudishwa.”[2]

al-Bukhaariy amepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu wote utaingia Peponi isipokuwa yule asiyetaka.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni nani atayekataa?” Akasema: “Yule mwenye kunitii, ataingia Peponi, na yule mwenye kuniasi amekataa.”[3]

al-Bukhaariy amepokea kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wanaochukiwa zaidi na Allaah ni watatu; mtenda dhambi Haram, mwenye kutaka katika Uislamu mwenendo wa kipindi cha kikafiri na mwenye kuomba damu ya mtu muislamu pasi na haki ili amwage damu yake.”[4]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mwenendo wa kipindi cha kikafiri inahusu kila kitu cha kipindi cha kikafiri, kisichofungwa au kisichokufungamana kwa mtu kama myahudi, mnaswara, mwabudia sanamu au mwingine mwenye kwenda kinyume na yale waliyokuja nayo Mitume.”

al-Bukhaariy amepokea kutoka kwa Hudhayfah ambaye amesema:

“Enyi wanazuoni! Bakieni katika njia iliyonyooka! Mkifanya hivo basi hakika mtakuwa mmetangulia mbele. Na mkienda kuliani na kushotoni basi hakika mmepotea upotevu wa mbali kabisa.”[5]

Muhammad bin Wadhdhwaah ameeleza jinsi Hudhayfah alivyokuwa akiingia msikitini na akiyasema haya. Akasema:

“Sufyaan bin ´Uyaynah ametueleza, kutoka kwa Mujaalid bin Sa´iyd, kutoka kwa ´Aamir ash-Sha´biy, kutoka kwa Masruuq ambaye ameeleza kuwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hakuna mwaka unaokuja isipokuwa ulio baada yake ni mbaya zaidi. Simaanishi kuwa kuna mwaka wenye kunyesha zaidi kuliko mwingine au wenye rotuba zaidi kuliko mwingine wala kiongozi ambaye ni bora kuliko mwingine. Ninachomaanisha ni kuondoka kwa wanazuoni wenu na wabora wenu. Kisha kutajitokeza watu ambao watayakisia mambo kwa matamanio yao ambapo watauharibu Uislamu na uangamie.”[6]

[1] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).

[2] Muslim (1718).

[3] al-Bukhaariy (7280).

[4] al-Bukhaariy (6882).

[5] al-Bukhaariy (7282).

[6] al-Bid´ah, uk. 61-62.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-ul-Islaam, uk. 10-12
  • Imechapishwa: 23/10/2016