2. Mazuri ya ndoa


Ndoa inampa mtu utulivu katika nafsi na furaha kwenye moyo. Inalinda utakaso, inahifadhi heshima na kushusha macho. Ni yenye kheri kwa mtu mwenyewe na jamii. Ina sifa na tofauti kubwa. Inafanya Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuongezeka na ujifakhirishaji wake na nyumati zingine juu ya idadi yenye wafuasi wengi siku ya Qiyaamah.

Ndoa ndio sababu ya kubaki kwa uanaadamu. Ndoa ndio njia yenye kujenga urafiki na ushirikiano kati ya watu wa jamii. Inaeneza mapenzi kati ya wanafamilia. Inafanya mioyo kuwa na ukaribu na kupunguza umbali. Ni familia ngapi zisizojuana isipokuwa ni kutokamana na umbali. Wakati wanapooana ndipo wanapojongeleana na inakuwa kana kwamba ni familia tu moja.

Kwa jumla ndoa ni yenye manufaa matupu na nguzo ambayo jamii imesimama juu yake. Kwa ajili hiyo Uislamu umekuja na kila chenye kuimarisha mapenzi kati ya wanandoa. Kwa sababu ndoa katika Uislamu inahusiana na mahaba, kuhurumiana na mapenzi. Ndoa katika Uislamu inahusiana na amani yenye kujaa kwenye nafsi, hisia zenye kujaa furaha na utulivu wa moyo.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 8-9
  • Imechapishwa: 21/03/2017