2. Imani na Uislamu ni nini na ni ipi misingi yake?


Swali 2: Ni nini imani na Uislamu na ni ipi misingi yake?

Jibu: Imani ni usadikishaji wa kuazimia yale yote ambayo Allaah na Mtume Wake wameamrisha kuyasadikisha. Usadikishaji wa kuazimia huo ndani yake mna kitendo. Kitendo hicho ndio Uislamu ambao maana yake yake ni kujisalimisha kwa Allaah peke yake na kunyenyekea Kwake kwa kumtii.

Kuhusiana na misingi yake ni ile ilio katika Aayah hii tukufu ifuatayo:

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ

”Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quub na al-Asbaatw na aliyopewa Muusa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.” (02:136)

Katika hiyo kunaingia pia yale aliyofasiri Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Jibriyl na wengine pale aliposema:

”Imani kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.”

Amesema pia:

”Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga ramadhaan na kuhiji Nyumba kwa yule mwenye kuweza kufanya hivo.”[1]

[1] Muslim (01).

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 21
  • Imechapishwa: 25/03/2017