19. Malengo ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kutunga kitabu hiki


Vitenguzi vya Uislamu – kama ilivyotangulia – ni yale mambo yanayouharibu na kuubatilisha. Yule mwenye kusilimu na akashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, Uislamu na Tawhiyd yake vinaweza kutenguka kwa kitenguzi moja wapo miongoni mwa vitenguzi hivi na huku anajua au hajui. Matokeo yake anaweza mwenye kuritadi na anakuwa katika idadi ya makafiri.

Vitenguzi vya Uislamu ni vingi. Kuna ambao wameyafikisha mpaka mia nne. Lakini yaliyo muhimu na khatari zaidi ni haya mambo kumi ambayo ameyataja Shaykh na Imaam na Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Lengo lake anautakia Ummah kheri na kuchelea juu ya Ummah wa Muhammad usije kutumbukia ndani yake. Ameyaandika na kuyaweka wazi kwa sababu ya kuutakia Ummah kheri, kuwa na khofu juu yake na kuuonea huruma. Na si kwamba anawakufurisha waislamu, kama wanavosema maadui na wapinzani wake, isipokuwa anawapa nasaha waislamu, kuwakumbusha na kuwafunza ili wajiepushe nayo na wajiweke nayo mbali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 26/06/2018