Swali 19: Mimba ikishakuwa na umbile la mtu na kukabaini kasoro ya kimaumbile na muumbuko katikati ya ile miezi ya ujauzito – je, inafaa kuiporomosha?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Ni lazima kuiacha. Allaah anaweza kuibadilisha. Madaktari wanaweza kudhania mengi na Allaah akazibatilisha dhana zao na matokeo yake mtoto akatoka salama salimina. Allaah anawajaribu waja Wake kwa furaha na yenye madhara. Haijuzu kuporomosha mimba kwa sababu tu imemdhihirikia daktari kwamba mtoto ana muumbuko. Ni lazima kuiacha kama ilivyo. Akiwa na muumbuko ashukuriwe Allaah wazazi wake watamlea na kumvumilia. Watapata thawabu nyingi katika jambo hilo. Wanaweza vilevile kumpeleka katika nyumba ya uangalizi ambayo nchi imetenga kwa ajili ya watu hao. Hakuna neno akafanya hivo. Mambo yanaweza kubadilika katika mwezi wa tano au wa sita wakadhani kuwa mtoto ana muumbuko kisha baadaye mambo yakabadilika na Allaah akamponya na zikaondoka sababu za muumbuko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 42
  • Imechapishwa: 04/08/2019