18. Kauli ya haki kuhusu imani


Kwa haya itapata kubainika maana ya Irjaa´ na kwamba ni kule kuchelewesha matendo nje ya imani, kwamba matendo hayaingii ndani ya imani, kwamba mtu anakuwa muumini ingawa hakufanya matendo kama vile kuswali, kufunga, kuhiji au matendo mengine yoyote. Iwapo atafanya ya kufanya katika maasi na katika madhambi ya kuangamiza bado ni muumini na maasi hayo hayaipunguzi imani yake. Wanaona kuwa endapo mtu atazini na kuiba ni muumini mwenye imani kamilifu muda wa kuwa ni mwenye kusadikisha kwa moyo wake.

Wanaona kuwa imani haishindani na wala haitofautiani. Wanaona kuwa imani ya Abu Bakr na Jibiyl ni kama imani ya mtu ambaye ni muovu kabisa katika watu.

Haki ni kwamba imani inashindana. Waumini wako miongoni mwao ambao imani yao ni kamilifu, miongoni mwao wako ambao imani yao ni pungufu upungufu mkubwa au upungufu mdogo. Imani inatofautiana, inazidi na inapungua. Inazidi kwa matendo mema na inapungua kwa maasi. Imani inaingia ndani ya uhakika wa imani. Mwenye kuacha matendo kabisa bila ya udhuru na asifanye matendo kamwe sio muumini. Lakini akiacha kufanya baadhi ya mambo na akafanya baadhi ya mambo yeye ni muumini mwenye imani pungufu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 37
  • Imechapishwa: 09/03/2021