18. Ameona mwezi mwandamao lakini hakuweza kuwafikishia serikali

Swali 18: Ni lazima kwa mtu kufunga ikiwa ana uhakika wa kuanza kwa mwezi mwanzoni lakini hata hivyo asiweze kuwafikishia taarifa mahakama?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana juu ya jambo hilo. Katika wao wako waliosema kuwa ni lazima kwake kufunga. Wengine wakasema kuwa halazimiki. Hilo ni kwa sababu mwezi mwandamo (الهلال) ni kitu kilichotangaa kati ya watu au kwamba mwezi mwandamo ni kitu kilichoonekana baada ya kuzama kwa jua. Ni mamoja kimetangaa kati ya watu au hakikutangaa.

Kinachonidhihirikia ni kwamba ambaye atauona na akawa na uhakika juu ya maono yake na wakati huohuo akawa katika maeneo ya mbali na hakushirikiana na yeyote katika kuuona au kuutafuta, basi itamlazimu kufunga. Hayo ni kutokana na ueneaji wa maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mkiuona, basi fungeni.”[2]

Lakini akiwa katika mji na akashuhudia mahakamani na ushahidi wake ukakataliwa, basi katika hali hii afunge kwa siri ili asitangaze kuwakhalifu kwake watu.

[1] 02:185

[2] al-Bukhaariy (1900) na Muslim (2471).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 21
  • Imechapishwa: 16/04/2021