173. Eda ya mwanamke aliyepotea mumewe kwa siku tatu

Swali 173: Mwanamke mmoja alimkosa mume wake na baada ya wiki akapatikana ameshakufa. Inaaminika kwamba alikufa siku tatu zilizopita. Ni lini ataanza kukaa eda; je, ni kuanzia ile tarehe alipotea, ni kuanzia ile tarehe ambayo alidhani kuwa amekufa au ni kuanzia ile tarehe aliyopopatikana[1]?

Jibu: Ni lazima kwake kuanza kukaa eda tangu pale alipopatikana amekufa. Kwa sababu hiki ndio chenye kuyakiniwa. Eda yake ni miezi minne na siku kumi. Ni lazima kwake kukaa eda. Isipokuwa akiwa mjamzito. Basi hapo muda wake wa eda utamalizika kwa kujifungua. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا

“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao [eda ya] miezi minne na siku kumi.”[2]

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

“Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”[3]

Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa fatwa Sabiy´ah al-Aslamiyyah alitoka ndani ya eda pale atapojifungua[4].

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/218-219).

[2] 02:234

[3] 65:04

[4] al-Bukhaariy (3691) na Muslim (2728).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 01/02/2022