17. Swalah ya ´Iyd


Miongoni mwa Sunnah asubuhi ya siku ya ´Iyd ni kuswali swalah ya ´Iyd na kutoa Zakaat-ul-Fitwr ili kumshukuru Allaah kwa ajili ya kutimiza swawm. Allaah ameifanya siku ya ´Iyd ni siku ya furaha kwa ajili ya kukamilisha ´ibaadah ya swawm kwa njia inayopasa inayotakiwa na Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo Allaah amewawekea Shari´ah waislamu watoke wende katika uwanja wa wazi na waswali swalah ya ´Iyd, wamtukuze Allaah na wamtaje ili wawe ni wenye kumshukuru Allaah (´Azza wa Jall) juu ya neema hii. Sikukuu zimewekwa katika Shari´ah kwa sababu hii.

Sikukuu nyengine zote zinazofanywa na watu hii leo ni sikukuu zilizozuliwa. Sikukuu za waislamu kwa mwaka ni mbili; ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa. Wana sikukuu vilevile kwa wiki, nayo ni siku ya ijumaa.

Tuna sikukuu tatu
kwa mwaka ni mbili; Fitwr na Adhwhaa ambayo ndio ya pili
Ya tatu ni yenye kujirudi kwa wiki
Hili lipo katika dini yetu tu hivyo basi jiandae

Hii ni fadhila ambayo Mtume wetu amefanywa kupwekeka nayo
ni nyumati ngapi zilizotangulia zimepotoshwa kutokamana nayo!
Zote zimefikiwa kwa kumshukuru Mneemeshaji
ambaye ameamrisha ´ibaadah kwa manufaa ya waislamu

Sio sikukuu zilizo na upuuzi na nyimbo
na sio kupoteza wakati pasi na faida

Ndio ni sikukuu, lakini zisizo na upuuzi, nyimbo na michezo. Zimewekwa kwa ajili ya kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 02/06/2017