192 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nisikujuzeni juu ya ambacho Allaah hufuta makosa na akapandisha kwacho ngazi?” Wakasema: “Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Kueneza maji vizuri katika kipindi kizito, hatua nyingi kwenda msikitini na kusubiri swalah moja baada ya swalah nyingine. Hiyo ndio kuchunga mipaka ya nchi, hiyo ndio kuchunga mipaka ya nchi, hiyo ndio kuchunga mipaka ya nchi.”[1]

Ameipokea Maalik, Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah kwa maana kama hiyo.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/195-196)
  • Imechapishwa: 15/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy