17. Bid´ah ni nini na ni vyepi vigawanyo vyake?

Swali 17: Bid´ah ni kitu gani na ni vyepi vigawanyo vyake?

Jibu: Bid´ah ni kwenda kinyume na Sunnah. Imegawanyika aina mbili:

1- Bid´ah ya kiitikadi. Ni kuwa na I´tiqaad kinyume na yale aliyoelezea Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imetajwa katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ummah wangu utagawanyika katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni ipi hiyo, Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”[1]

Ambaye yuko katika wasifu kama huu basi anafuata Sunnah safi. Anayefuata mapote mengine ni mzushi. Kila Bid´ah ni upotevu na zinatofautiana kwa kiasi na zilivyo mbali na Sunnah.

2- Bid´ah ya kimatendo. Ni kule kuabudu kwa njia ambayo haikuweka Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kuharamisha kitu ambacho Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamehalalisha. Hivyo yule mwenye kuabudu kwa njia ambayo haikuwekwa katika Shari´ah au akaharamisha kitu ambacho dini haikuharamisha, ni mzushi.

[1] at-Tirmidhiy (2641) na al-Haakim (1/128).

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com