16. Unafiki ni kitu gani na umegawanyika sehemu ngapi na sifa zake?


Swali: Unafiki ni kitu gani na umegawanyika sehemu ngapi na zipi sifa zake?

Jibu: Unafiki maana yake ni kuficha kheri na kuficha shari. Umegawanyika aina mbili:

1- Unafiki mkubwa wenye kuhusiana na imani. Aliye na unafiki aina hii atadumishwa Motoni milele. Mfano wake ni kama yale aliyoelezea Allaah kuhusu wanafiki pale aliposema:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ

“Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho”, hali ya kuwa si wenye kuamini.” (02:08)

Hawa wanaficha ukafiri na wanaonesha imani.

2- Unafiki mdogo wenye kuhusiana na matendo. Mfano wake ni kama yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Alama za mnafiki ni tatu; anapozungumza husema uongo, anapoahidi hatimizi na anapoaminiwa anasaliti.”[1]

Kufuru na unafiki mkubwa haunufaishi imani na matendo. Kuhusu kufuru na unafiki mdogo, unaweza kukusanyika sehemu moja na imani. Katika hali hii mja anakuwa na kheri na shari na anastahiki thawabu na adhabu vyote viwili.

[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (59).