16. Udugu kati ya Muhaajiruun na Answaar

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaandikiana mkataba wa amani na mayahudi waliopo al-Madiynah. Mwanachuoni wao ´Abdullaah bin Salaam (Radhiya Allaahu ´anh) akaingia katika Uislamu wakati wengi wao wakakufuru. Mayahudi walikuwa makabila matatu; Qaynaqaa´, an-Nadhwiyr na Quraydhwah.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya udugu kati ya Muhaajiruun na Answaar. Mwanzoni mwa Uislamu walikuwa wakirithiana kwa udugu huu badala ya udugu.

Wakati huo Allaah (´Azza wa Jall) akafaradhisha zakaah ili kuwafanyia wepesi mafakiri wa Muhaajiruun. Hivyo ndivyo alivyosema Ibn Hazm katika kitabu chake cha historia. Baadhi ya wanachuoni wa Hadiyth wamesema kuwa hawajui ni lini zakaah ilifaradhishwa.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 39
  • Imechapishwa: 18/03/2017