18. Kuwasaidia washirikina dhidi ya waislamu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

08 – Kuwasaidia washirikina [makafiri] dhidi ya waislamu. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.”[1]

MAELEZO

Muislamu akawasaidia makafiri dhidi ya waislamu. Kwa mfano kama kuna vita kati ya waislamu na makafiri halafu akawasaidia na kuwasapoti makafiri hawa katika kuwapiga vita waislamu. Ni mamoja akawasaidia kwa pesa, silaha au akawapangia rai za vitimbi. Akiwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ili waweze kupata njama basi anakuwa kafiri. Kwa sababu amewafadhilisha makafiri juu ya waislamu. Ufadhilishaji huu unapelekea kwamba mtu huyo anauchukia Uislamu, Allaah na Mtume Wake. Yule mwenye kumchukia Allaah (´Azza wa Jall), Mtume Wake au chochote katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi anakuwa kafiri. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

“Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale aliyoyateremsha Allaah, basi akayaporomosha matendo yao.”[2]

Asiyempenda Allaah na Mtume Wake ni kafiri. Ni lazima kupatikane ule msingi wa mapenzi. Lakini kuhusu ukamilifu, kwa msemo mwingine kile kitendo cha mtu kutanguliza mapenzi ya kumpenda Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya mke, watoto na mali, huu ndio ukamilifu tunaokusudia. Mwenye kutanguliza kitu katika mali, mke au kitu kingine juu ya mapenzi ya kumpenda Allaah na Mtume Wake anakuwa ni mtenda dhambi ambaye imani yake ni pungufu. Lakini asipompenda Allaah na Mtume Wake anakuwa kafiri. Anayewasaidia makafiri dhidi ya waislamu hampendi Allaah na Mtume Wake. Kinyume chake ni mwenye kuwachukia na kuchukia yale aliyoteremsha Allaah. Hivyo anaingia katika maneno Yake (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

“Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale aliyoyateremsha Allaah, basi akayaporomosha matendo yao.”

Dalili nyingine maalum yenye kuonyesha kuwa kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ni ukafiri ni Aayah hii Tukufu katika Suurah al-Maaidah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚوَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara kuwa ni marafiki – wao kwa wao ni marafiki. Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.”[4]

Tawalliy (التولي) ni kuwapenda washirikina. Kitendo hichi ni ukafiri na kuritadi. Mapenzi haya yanazalisha kuwasaidia dhidi ya waislamu. Kwa hiyo yule mwenye kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ni dalili tosha ya kwamba anawapenda makafiri, kitendo ambacho ni kuritadi.

[1] 05:51

[2] 47:09

[3] 47:09

[4] 05:51

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 15/04/2023