16. Mwisho wa kitabu “al-Qadhwa´ wal-Qadar”

Tunamalizia kwa kusema ni lazima kwa muumini aridhie kuwa na Allaah kama Mola. Ina maana vilevile ya kwamba aamini mipango na makadirio ya Allaah na atambue kuwa hakuna tofauti kati ya matendo anayoyafanya na bidii ya kutafuta riziki na kutaka kukwepa muda wa kueshi uliyopangwa. Yote hayo ni sawa sawa. Yote yameandikwa. Yote yamekadiriwa. Kila mtu ni mwenye kusahilishiwa kwa kile alichoumbiwa kwacho.

Ninamuomba Allaah (´Azza wa Jall) atufanye miongoni mwa wenye kusahilishiwa matendo ya wale wenye furaha na atuandikie wema wetu duniani na Aakhirah. Himdi zote zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake.

Mwisho na himdi zote zinamstahikia Allaah (Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/227)
  • Imechapishwa: 25/10/2016