16. Dalili ya kumi na nne kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

15- ´Ubayd al-Muktib amepokea kutoka kwa Mujaahid ambaye amesimulia kwamba ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Hakika Allaah ameumba vitu vine kwa mkono Wake: Aadam, kalamu na mabustani ya Edeni. Akaviambia viumbe vyengine vyote “Kuwa!” na vikawa.”[1]

Wameipokea zaidi ya mmoja kutoka kwa ´Ubayd, akiwemo Sufyaan ath-Thawriy na ´Abdul-Waahid bin Ziyaad.

[1] al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (693), al-Haakim (2/319), ash-Shariy´ah, uk. 313, na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 20/06/2019