16- ´Aliy bin Abiy Twaalib ametuhadithia: ar-Raffaa´ ametuhadithia: Bishr bin Muusaa ametuhadithia: ´Abdullaah bin az-Zubayr ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: ´Amr bin Diynaar ametuhadithia: ´Amr bin Aws amenihadithia ya kwamba alimsikia ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) akieleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waadilifu watakuwa juu ya mimbari za nuru upande wa mkono wa kulia[1] wa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) na mikono Yake yote ni ya kuume.”[2]

[1] Imaam Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

”Uhakika wa mambo ni kwamba mtu hawezi kumthibitishia wala kumkanushia upande Allaah (Ta´ala) likitajwa pasina kufungamanishwa. Katika hali hiyo swali ni lazima lifafanuliwe. Ikiwa upande wa chini ndio makusudio, basi ni jambo lisilowezekana kwa Allaah. Bali haiwezekani kwa Allaah (Ta´ala) akasifika kwayo. Ni lazima Allaah (Ta´ala) asifike na ujuu kabisa kuhusiana na dhati na sifa Zake. Ikiwa upande wa juu unaomfunika ndio makusudio, Allaah hasifiki nao. Bali ni jambo lisilowezekana kwa Allaah (Ta´ala) kusifika nao. Allaah ni Mkubwa na Mtukufu zaidi kufunikwa na kitu katika viumbe Wake. Itakuweje ilihali Kursiy yake imezunguka mbingu na ardhi?

وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Ataikamata ardhi yote siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia.” (39:67)

Ikiwa makusudio ni upande wa juu wenye kulingana na ukubwa na utukufu Wake pasi na lengo la kumzunguka, hiyo ni haki na ndio imethibiti kwa Allaah (Ta´ala) na ni wajibu asifiwe nao. Shaykh Muhammad ´Abdul-Qaadir al-Jaylaaniy amesema katika kitabu chake “al-Ghunyah”:

“Yeye (Subhaanah) yuko katika upande wa juu. Amelingana juu ya ´Arshi na yuko na ufalme.” (Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 39)

[2] Muslim (1827).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 39-42
  • Imechapishwa: 20/01/2017