Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ

“Hakika mfano wa uhai wa dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uwezo juu yake tahamaki amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofekwa kama kwamba haikusitawi jana.” (10:24)

اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖكَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ

“Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na wana. Ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka. Na Aakhirah kuna adhabu kali na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhina uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe zenye kudanganya.” (57:20)

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَلَكَهُ يَنَابِيعَ فِي الْأَرْضِ ثُمَّ يُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَجْعَلُهُ حُطَامًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ

“Je, huoni kwamba Allaah anateremsha kutoka mbinguni maji akayapitishia chemchemu katika ardhi, kisha anatoa kwayo mimea ya rangi mbalimbali, kisha hunyauka, basi utayaona ni manjano, kisha huyafanya kumeng’enyeka. Hakika katika hayo bila shaka kuna ukumbusho kwa wenye akili.” (39:21)

220- adh-Dhwahhaak bin Sufyaan amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinambia: “Ee adh-Dhwahhaak! Unakula nini?” Nikajibu: “Nyama na maziwa.” Akauliza: “Kisha unakuwa vipi?” Nikajibu: “Inakuwa vile unavyojua, ee Mtume wa Allaah.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Allaah amefanya kila kinachomtoka mwanaadamu ndio mfano wa dunia hii.”[1]

221- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Chakula cha mwanaadamu kinafanana na dunia hata kama atakitia viungo na chumvi; atazame baadae kinakuwa vipi.”[2]

[1] Ahmad (3/452). Tazama ”as-Silsilah as-Swahiyhah” (382) ya al-Albaaniy.

[2] Ibn Hibbaan (2489). Tazama ”as-Silsilah as-Swahiyhah” (382) ya al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 128-129
  • Imechapishwa: 18/03/2017